Ile mechi kali ya wakali wa shule ya sekondari ENGUTOTO yaani kidato cha Tano na kile cha Sita inatarajia kupigwa leo shuleni Engutoto
Mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu unatarajia kuanza majira ya saa kumi na nusu jioni ambapo wadau mbali mbali wa soka shuleni hapa wanawapa kidato cha tano nafasi ya kushinda
akizungumza mbele ya waandishi wa blog hii mwalimu wa michezo shuleni hapa Richard Ngoda alisema ''kidato cha tano wanaonekana kuimarika sana kuliko kidato cha sita na hivyo nawapa nafasi ya kushinda tena kwa kishindo'' aidha kwa upande wao wachezaji kidato cha sita wamekiri kuwa na hofu sana na mechi hii tofauti kabisa na wenzao kidato cha tano
habari na mwandishi wetu Pasco Nkololo & Malogi Kusekwa
No comments:
Post a Comment