Friday, 31 October 2014

ENGUTOTO SECONDARY SCHOOL

Engutoto secondary ni shule inayopatikana katika mkoa wa arusha ,wilaya ya monduli
shule hii inafahamika kote Tanzania kutokana na historia nzuri iliyonayo
shule hii ni ya kutwa na bweni na ya mchanganyiko wavulana na wasichana Mwalimu mkuu wa shule hii anaitwa LOMAYANI SAILEPU akisaidiana na makamu mkuu wa shule hii bw WILLIAM WALTER shule ina wanafunzi wa O-LEVEL na wale wa A-LEVEL kwa michepuo ya HKL,HGL,na HGK kwa kifupi ni kwamba shule imekua na mfululizo wa matokeo mazuri kwa mitihani ya taifa kwa miaka mingi mfululizo na hivyo kuzidi kuwa chachu ya maendeleo katika mkoa wa arusha na taifa kwa ujumla

Habari na mwandishi Pasco Nkololo

Sunday, 26 October 2014

TUMEDHAMIRIA KUSHIKA HATAMU KITAALUMA

Makamu mkuu wa shule ya sekondari ENGUTOTO Ndg William Walter akifafanua jambo wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapa ambayo ililenga kufanya mapinduzi ya kitaaluma shuleni hapa
katika hafla hiyo mambo mengi yaliafikiwa ikiwemo la kuhakikisha ENGUTOTO inabaki katika ramani ya juu kabisa kitaaluma katika mkoa wa arusha na taifa kwa ujumla

Habari na Picha na mwandishi wetu Stephano Mahelu

waziri mkuu mstaafu katika moja ya ziara zake shuleni ENGUTOTO

Hapa akizungumza na wanafunzi wa kidato cha sita 2014 shuleni hapa

Official;Engutoto secondary school yazindua blog yake

Shule ya sekondari ENGUTOTO imezindua rasmi blog yake ambayo itawasaidia walezi na wazazi wa wanafunzi wake kujua mambo mbali mbali yanayofanyika shuleni hapa mambo hayo ni pamoja na
                      -Habari mbali mbali kuhusu ENGUTOTO
                      -Matokeo ya mitihani (examinations results)
                      -picha na video mbali mbali
                      -forms za kujiunga na engutoto (joining instructions)
                      -na mengine mengi yahusuyo ENGUTOTO
Blog hiyo ambayo imetengenezwa na mwanafunzi PASCO NKOLOLO inatarajiwa kuwa chachu kubwa ya maendeleo katika shule hii hivyo ni rai kwa wanajamii wa ENGUTOTO SECONDARY kuzidi kuunga mkono jitihada za shule hii ili izidi kuwa mfano popote tanzania

Saturday, 25 October 2014

ENGUTOTO NI FULL VIPAJI

WACHEZAJI WA STAFF YA ENGUTOTO SECONDARY WAKIWA TAYARI KWA MOJA KATI YA MICHEZO YAO SHULENI HAPO

EXCLUSIVE; RATIBA MTIHANI WA ANNUAL NA TERMINAL HEWANI

Ratiba ya mtihani kwa vidato vya tano,tatu,na kile cha kwanza imetolewa rasmi na ofisi ya taaluma shule ya sekondari ENGUTOTO.
Mitihani inategemea kuanza rasmi tarehe 17/11/2014 kwa vidato tajwa.Pia unategemea kumalizika tarehe 22/11/2014 ambayo ni tarehe rasmi kwa kidato cha sita kuanza mtihani  wao wa Mock.
 
  Mwalimu mkuu wa taaluma shuleni hapa bw.Nathanael Mungule alisema ofisi ya taaluma na shule nzima kwa ujumla wanategemea ufaulu wa hali ya juu katika mitihani hiyo kama ilivyo desturi ya ENGUTOTO SECONDARY

''all we need is you to have aattractive and best perfomance as ussual'' alisema
na kwa upande wao wanafunzi wa kidato cha tano shuleni hapa wameahidi kufanya vema ktk mitihani hiyo

Friday, 24 October 2014

ENGUTOTO SECONDARY YAWAPIGISHA KWATA WAJESHI WA T.M.A

Timu ya soka ya engutoto imefanikiwa kuichapa kwa mabao matatu kwa bila timu ya soka ya T.M.A katika mchezo wa kirafiki uliofanyika shuleni hapo jioni hii

 mabao ya ENGUTOTO yaliwekwa kimiani na mshambuliaji wao hodari Chendwa Isaya na Mwalimu Khamis huku mabao yote yakitengenezwa na kiungo mshambuliaaji John Sandu

Kikosi cha engutot leo hii kilikua
1;Manyonyi Matofali
2;Peter Mwanza
3;Novatus
4;Richard John
5;Musa msape
6;Edom Minja
7;Mwalimu Khamis
8;Master Makundi
9;Chendwa Isaya
10;John Sandu
11;Darl Darlius

 Kwa niaba ya familia ya wana ENGUTOTO tunasema

HONGERENIIIIIIIIIIIII

ENGUTOTO HIGH SCHOOL KITOVU CHA KITAALUMA KATIKA MKOA WA ARUSHA

Shule ya sekondari engutoto iliyopo mkoani arusha katika wilaya ya monduli imetajwa kuwa moja ya vitovu vya kitaaluma katika mkoa huo kutokana na mfululizo wa matokeo mazuri katka shule hiyo

Hayo yamesemwa na moja kati ya wadau wakubwa wa shule hiyo KISA PROJECT katika hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo siku ya ijumaa ya tar 24 shuleni hapo

HELLOW ENGUTOTO HIGH SCHOOL

Hellow engutoto high school.this is our new blogg.this blogg tells about how Engutoto High school is,it's location, description and other more concerned with youth around Engutoto High school.